Ataba yatoa pole kwa familia ya shahidi wa fatwa

Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa pole kwa familia ya shahidi Qassim Hussein Almaliki (r.a) aliyepata shahada katika opresheni ya Mosul, baada ya kuhudhuria kwenye majlisi ya taazia iliyofanywa katika mkoa wa Bagdad.

Makamo rais wa kitengo cha mahusiano Sayyid Muhammad Swadiq Jalukhani amesema “Kwa maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d,i) na katibu mkuu Sayyid Muhammad Murtadha Dhiyaau-Dini, tumehudhiria majlisi ya taazia ya shahidi Qassim Almaliki aliyekua mpiganaji wa kikosi cha Answaru-Marjaiyya kuipa pole familia yake”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imetoa msaada wa kimaana na kimada kwa familia ya shahidi pamoja na kukabidhi bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Shahidi Qassim Almaliki aliitikia wito wa fatwa ya Marjaa Dini mkuu mwaka 2014m, hadi alipopata shahada katika kulinda taifa lake na maeneo matakatifu tarehe 18 mwezi huu kwenye opresheni ya Mosul (Alhadhar).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: