Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake imeanza kupokea washiriki wa semina za Qur’ani

Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kupokea washiriki wa semina za Qur’ani baada ya kuisha likizo ya ziara ya Arubaini.

Kiongozi wa Maahadi hiyo bibi Manaar Aljaburi amesema: “Maahadi imeanda kupokea wanafunzi wa semina za Qur’ani baada ya kuisha likizo ya ziara ya Arubaini, ambapo ratiba ya masomo ni asubuhi na jioni katika ofisi za Maahadi mjini Najafu”.

Akaongeza kuwa “Maahadi inaendelea na kazi zake na imekusudia kufungua semina mpya itakayo husisha idadi kubwa ya wasichana wanaopenda kujifunza Qur’ani”.

Akafafanua kuwa “Maahadi inatoa semina bure kwa wasichana, pamoja na kuwapa usafiri wa kuwachukua na kuwarudisha nyumbani kwao, kwa lengo la kuelimisha kundi hilo muhimu katika jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: