Zaidi ya watu milioni nne wamenufaika na huduma ya kitengo cha mgahawa katika ziara ya Arubaini

Idadi ya wanufaika wa kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya wakati wa ziara ya arubaini ni watu (4,134,881).

Kitengo cha mgahawa kimesema: “Huduma zilizotolewa na kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wa ziara ya Arubaini katika mji wa Karbala ni ugawaji wa chakula siku zote za ziara”, akafafanua kuwa “Watu waliopewa chakula ni mazuwaru, wahudumu wa kujitolea, wageni wa Ataba na watumishi wa Ataba tukufu”.

Kitengo kimesisitiza katika tamko lake kuwa “Jumla ya wanufaika ni (4,134,881) milioni nne laki moja thelathini na nne elfu mia nane themanini na moja”.

Kwa mujibu wa tamko hilo, kitengo cha mgahawa kiliendelea kugawa chakula hata baada ya kuisha ziara ya Arubaini kutokana na kuendelea kumiminika wageni katika mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: