Markazi Dirasaati Afriqiyya inajadili njia za kusaidiana na ugeni kutoka Seralion

Markazi Dirasaati Afriyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea wageni miongoni mwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutoka nchini Seralion, uliohusisha mubaligina, watafiti na mahafidh wa Qur’ani tukufu.

Rais wa Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni Shekhe Saadi Sataari Shimri amesema: “Hakika kikao kimehusisha viongozi tofauti wa Markazi, tumekubaliana kutekeleza ratiba za kitablighi, Qur’ani na kibinaadamu katika miji tofauti nchini Seralion”.

Akabainisha kuwa “Tumejadili namna ya kushirikiana katika kutekeleza ratiba ya Tablighi, Markazi itachinmba kisima kupitia mradi wake wa mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi Atwaasha Karbala), pamoja na kufanya semina za kidini kwenye miji tofauti ya Seralion, ambapo Markazi itasimamia na kufadhili”.

Akafafanua kuwa “Kuna kundi kubwa la wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Seralion wenye kiu ya kutambua uislamu halisi wa Mtume wetu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: