Maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel inajiandaa kutoa huduma katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume mtukufu

Maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel imekamilisha maandalizi ya kutoa huduma kwa mazuwaru wanaoenda kwenye malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu kuomboleza kifo cha Mtume mtukufu (s.a.w.w).

Rais wa chuo hicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Nurisi Dahani amesema: “Maukibu yetu hutoa huduma katika mkoa wa Najafu, jambo hilo hupewa umuhimu mkubwa na Ataba tukufu”.

Akabainisha kuwa “Maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel ilianzishwa sambamba na kuanzishwa kwa chuo, na ikatumia jina la chuo, imekuo ikiongeza huduma zake kila mwaka”.

Kwa mujibu wa Dahani: “Maukibu imeweka kambi kwenye barabara ya Imamu Ali (a.s) inayo elekea Haram tukufu mkabala na sehemu ya kupumzika ya Atabatu Alawiyya, hushiriki kutoa huduma kwenye ziara nyingi kubwa zinazofanywa katika mkoa wa Najafu, ikiwemo ziara hii tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: