Kituo cha tafiti na rejea za kielimu kinaendelea na harakati yake ya kijamii na kielimu

Kituo cha tafiti na rejea za kielimu kinaendelea na harakati yake katika mji mkuu wa Bagdad baada ya kusimama wakati wa ziara ya Arubaini, kimetoa mihadhara miwili kwa wanafunzi.

Mkuu wa kituo cha utafiti na rejea za kielimu Ustadh Hassan Aljawadi amesema “Baada ya kusimama harakati zetu kwa ajili ya ziara ya Arubaini, kituo kimeanza tena harakati kwa kutoa mihadhara miwili katika mkoa wa Bagdad kwa wanafunzi wa shule za sekondani (upili) kwa kushirikiana na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Shekhe As’adi Zubaidi”.

Akaongeza kuwa: “Shekhe Hussein Isawi alitoa mhadhara wa kwanza usemao (Uhakika wa elimu na umuhimu wa kusoma) akabainisha nukta mbalimbali zinazoonyesha umuhimu wa elimu na faida yake katika maisha”.

Kuhusu mhadhara wa pili “Ameongea wakati mzuri wa kusoma na jinsi ya kupanga muda kwa kundi hili muhimu la wanafunzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: