Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa wito kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kuhudhuria kwenye hafla ya kukamilika kwa dirisha jipya la malalo ya bibi Zainabu (a.s), lililotengenezwa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya, itakayo fanyika muda mfupi kabla ya kulibeba na kulipeleka kwenye malalo yake takatifu nchini Sirya.
Hafla itafanywa kwenye uwanja wa mbele ya mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kulitoa kwenye kiwanda cha madirisha ya makaburi saa kumi na moja jioni siku ya Jumanne mwezi 30 Safar 1444h sawa na tarehe 27/09/2022m.