Majmaa ya Qur’ani tukufu imefanya hafla ya kwanza katika mradi wa mahafali za Ain

Majmaa ya Qur’ani tukufu imefanya kikao cha kwanza cha usomaji wa Qur’ani katika mradi wa vikao vya usomaji wa Qur’ani vya kila mwezi kwenye ofisi za Ain zilizopo Kadhimiyya.

Kikao hicho kimesimamiwa na kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya kwa mujibu wa kiongozi wa idara ya Qur’ani Wahaji Abadi.

Amesema: “Hafla imefanywa sambamba na kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)”, akaongeza kuwa “Wasomaji wa Qur’ani katika Ataba mbili tukufu bwana Osama Karbalai na Muhammad Ridha Zubaidi wamesoma Qur’ani katika hafla hiyo”. Akasema “kulikua na usomaji wa utenzi mwisho wa hafla”.

Kuhusu vikao vingine vya usomaji wa Qur’ani amesema “Vitaandaliwa vikao vingine vya usomaji wa Qur’ani baada ya mwezi wa Safar kwenye makao makuu ya Ain na matawi yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: