Chuo kikuu Alkafeel katika mji mtukufu wa Najafu kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Rais wa chuo hicho Dokta Nuris Dahani ambacho kipo chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya amesema “Tunatoa kipaombele cha kuadhimisha matukio ya Dini katika chuo hiki, kwani ni taasisi ya kimalezi na kielimu inayofuata mafundisho ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ya kujitolea na uaminifu”, akasema “kunaratiba maalum ya swala hilo ambapo hualikwa watafiti na wahadhiri mbalimbali kuja kuzungumza”.
Majlisi hiyo imehutumiwa na Sayyid Jafari Murawiji, ametaja mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa katika historia ya Mtume mtukufu.