Maukibu ya wahudumu wa Ataba mbili tukufu inaomboleza kifo cha Mtume Mtukufu

Siku ya Jumapili mwezi (28 Safar 1444h) baada ya Adhuhuri, maukibu ya kuomboleza inayoundwa na wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, imeenda kumpa pole bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Maukibu imeanzia matembezi yake ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ikapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu huku wanaimba kaswida za huzuni na kuomboleza msiba uliotokea katika nyumba wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Maukibu ilipowasili kwenye malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) ilipokewa na wahudumu wa Atabatu Husseiniyya tukufu, baada ya kuingia ndani ya haram Husseiniyya wakafanya majlisi ya kuomboleza ambayo mazuwaru walishiriki pia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: