Kitengo cha kusimamia haram tukufu kinafanya ukarabati wa taa za mapambo

Maoni katika picha: Moja ya taa za mapambo katika
Wahudumu wa kitengo cha kusimamia haram ya Atabatu Abbasiyya wanafanya ukarabati wa taa za mapambo zilizopo ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Makamo rais wa kitengo hicho Zainul-Aabidina Adnani Kuraishi amesema “Kitengo cha taa za mapambo kina idara tatu, idara ya ufungaji wa taa, idara ya matengenezo na idara ya usafi”.

Aidha kitengo kina kamati maalum ya mafundi wanaofanya kazi ya matengenezo kwa utaratibu maalum. Akafafanua kuwa “Kuna aina tofauti ya taa za mapambo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zipo za kwenye paa na ukutani na zinaukubwa tofauti”.

Taa hizo zimeagizwa kutoka moja ya nchi za ulaya, zilitengenezwa kwa oda, kila taa inanembo ya Ataba tukufu.

Kwa Mujibu wa Kuraishi, kitengo cha kusimamia Haram tukufu kinajukumu maalum katika Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama kufanya usafi, kutandika mazulia, kupuliza marashi na zinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: