Markazi Dirasaati Afriqiyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mkoa wa Kigoma uliopo magharibi ya nchi ya Tanzania.
Mkuu wa Markazi hiyo chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Markazi imefanya majlisi ya kuomboleza katika mkoa wa Kigoma magharibi ya Tanzania katika bara la Afrika, iliyohudhuriwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), wamefanya matembezi ya kuomboleza yaliyojaa huzuni na majonzi”.
Akaongeza kuwa “Mhadhara umehusu historia ya Maisha ya Mtume (s.a.w.w), utukufu wake na kazi kubwa aliyofanya ya kurekebisha jamii”.
Kwa mujibu wa Shimri: “Majlisi hiyo ni sehemu ya harakati za kiibada na kitablighi, chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.