ugeni wa Atabatu Abbasiyya katika mji wa Damaskas umemtembelea Mheshimiwa Shekhe Bahabahani muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu

ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika jiji la Damaskas umemtembelea muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani, Hujjat Islamu walmuslimina Shekhe Abdulhalim Bahabahani.

Rais wa ugeni huo Sayyid Jawadu Hasanawi amekiambia kituo cha Habari kuwa “Ziara ya Shekhe Abdulhalim Bahabahani, ililenga kumuonyesha kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu hapa Damaskas, kazi ya kufungua dirisha la zamani na kufunga jipya kwenye kaburi la bibi Zainabu Kubra (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Mheshimiwa Shekhe Bahabahani tumemuambia kwa urefu hatua za utengenezaji wa dirisha tukufu la bibi Zainabu (a.s), Pamoja na kufafanua utaratibu unaotumika katika kufungua na kufunga dirisha hilo tukufu, hivi sasa tupo katika ufungaji wa mbao zinazo zunguka kaburi la Hauraa Zainabu (a.s), kwa lengo la kuanza kazi ya kufungua dirisha la zamani na kufunga jipya lililo tengenezwa na watumishi wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kuwa “Ugeni kutoka Ataba tukufu baada ya kuwasiri katika malalo ya jabali wa Subira Hauraa Zainabu (a.s), kwa maelekezo ya mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, tulifanya kikao na watumishi wa Atabatu Zainabiyya na kujadili utaratibu wa kufungua dirisha la zamani na kufunga jipya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: