Toleo la hivikaribuni (Maneno mazuri katika hali za watu)

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha kitabu kiitwacho (Maneno mazuri katika hali za watu) kilicho andikwa na Faqiihi Shekhe Muhammad Twaha Najafu (q.s) aliyefariki mwaka (1323h).

Usimamizi wa kuchapishwa kitabu hicho umefanywa na kituo cha Shekhe Tusi chini ya kitengo cha uchapishaji wa vitabu kwa mujibu wa maelezo ya Shekhe Muslim Ridhaaiy, akasema: “Kitabu kimetokana na uhakiki wa Shekhe Muhammad Jafari Islami”.

Kitabu hiki ni miongozi mwa vitabu bora vya elimu ya Rijali kwa mujibu wa mkuu wa kituo, “Muandishi ametegemea wapokezi waaminifu na akabainisha nzuri na dhaifu, kwa kutumia mfumo wa utatu huku kitabu akikiweka katika sehemu tatu”.

Shekhe Ridhaaiy akaonyesha furaha ya kituo kwa kuchapishwa kitabu hiki kilicho hakikiwa kwenye juzuu nne, kikiwa na maelezo kutoka kwa Allamah Sayyid Hassan Swadri (r.a).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: