Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu wameshiriki kwenye wiki ya usafi hapa Karbala.
Makamo rais wa kitengo hicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Shaakir Hashim amesema “Kitengo kimechukua jukumu la kusafisha chochoro na barabara zinazozunguka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika wiki ya usafi wa Karbala”.
Akaongeza kuwa: “Kazi hii inafanywa baada ya kumaliza kipindi cha ziara iliyohudhuriwa na mamilioni ya watu, watumishi wa kitengo chetu wamechukua jukumu la kusafisha barabara zote zinazoelekea kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu pamoja na chochoro za mji wa zamani”.
Kazi zote zinafanywa kwa kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Karbala.
Watumishi wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, walikua wamesha fanya usafi kama huo mara tu baada ya ziara ya Arubaini, ambapo walisafisha (eneo la mlango wa Bagdad, barabara ya Hauraa-Zainabu, barabara ya Alqami, barabara ya Jannatul-Hussein, barabara ya Maosheo ya zamani, eneo la katikati ya haram mbili tukufu na barabara ya Maimamu wa Baqii) kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo.