Idara ya mawasiliano: Tunafanya kazi na vitengo vyote kupitia kamera

Ofisi ya kamera katika idara ya mawasiliano imesema kuwa inafanya kazi na idara zote kupitia kamera wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kiongozi wa idara hiyo chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi Mhandisi Farasi Abbasi Hamza amesema: “Kazi kubwa ya kamera ni ulinzi, sambamba na kufuatilia utendaji wa vitengo vya Ataba tukufu kama vile kitengo cha kulinda nidham na vituo vya ukaguzi”, akabainisha kuwa “Linapo tokea jambo lolote lisilo la kawaida hupewa taarifa kitengo cha kulinda nidham kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka zinazofaa kulingana na jambo lililotokea”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa taasisi kubwa na inaendelea kukua kila siku, miongoni mwa kukua kwake ni idara ya mawasiliano yenye jukumu la kuangalia utendaji wa vitengo vingine pia, sambamba na kuboresha sekta ya teknolojia na mawasiliano”.

Kuhusu maendeleo ya teknolojia, amesema: “Idara inatoa semina za kuwajengea uwezo watumishi wake mara kwa mara ndani na nje ya Iraq, sambamba na kushiriki kwenye maonyesho ya kielimu na kiteknolojia yanayo husu kompyuta na kamera”.

Kuhusu huduma zinazotolewa na kitengo hicho amesema kuwa “Teknolojia imesaidia kurahisisha jukumu la kuongoza waliopotea wakati wa ziara ya Arubaini”, akasisitiza kuwa “Imefanya kazi kubwa katika kutekeleza jukumu hilo muhimu la kumkutanisha mtu aliyepotea na jamaa zake katikati ya mamilioni ya watu, pamoja na kurahisisha mawasiliano na matumizi ya ukurasa wa taarifa na mambo mengine kwenye sekta ya mawasiliano”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: