Chuo kikuu cha Al-Ameed kimepokea kamati ya elimu kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, inayo undwa na wakufunzi wa vyuo, yenye jukumu la kupima kiwango cha elimu, ubora na usalama wa maabara.
Kamati hiyo inawajibu wa kukagua masomo na maabara kwenye vitivo vya famasia, uganga na uuguzi, chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ugeni huo umepokewa na wakuu wa vyuo na wasaidizi wao.
Kamati ya wizara imefanya ukaguzi kwenye vifaa vya kufundishia na maabara za chuo, sambamba na kukagua usalama wake na usalama wa kumbi za masomo na kiwango cha wanafunzi wanaofaa kukaa kwenye kila ukumbi wa darasa, pamoja na mambo mengine kulingana na kanuni za wizara.