Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya warsha kuhusu namna ya kuamiliana na mtu aliyekasirika

Kitengo cha kuongoza nafsi na malezi katika chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya warsha iliyopewa jina la “Idara ya hasira na namna ya kuamiliana na mtu aliyekasirika”.

Mtoa mada kwenye warsha hiyo ni mkuu wa kitengo cha kuongoza nafsi Dokta Husaam Ali Ubaidi na washiriki ni watumishi wa uelekezaji na wanaofanya kazi kwenye ofisi za mapokezi chuoni.

Amezungumza kuhusu athari ambazo hutokea iwapo mtu atashindwa kuzuwia nafsi yake, na njia zinazo weza kusaidia kumiliki hisia anapoamiliana na mtu aliyekasirika.

Warsha hii ni sehemu ya ratiba ya mihadhara iliyoandaliwa na kitengo cha kukuza vipaji kwenye mkakati wa mwaka huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: