Sayyid Swafi amzawadia mmoja wa wanafunzi aliyehifadhi vizuri miongoni mwa mahafidhi wa Majmaa-Ilmi

Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amempa zawadi mwanafunzi Abbasi Maitham Abbasi aliyehifadhi Qur’ani tukufu katika Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya, chini ya Majmaa-Ilmi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mwanafunzi huyo ni miongoni mwa waliofaulu kwenye mtihani wa darasa la sita kwa kupata alama (99.14) kwenye mtihani wa mwisho wa mwaka.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya ambao ni Sayyid Liith Mussawi, Dokta Mushtaqu Ali rais wa kitengo cha Majmaa-Ilmi ya Qur’ani na kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abi.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani itafanya hafla ya kumpongeza mwanafunzi huyo Abbasi katika malalo ya Sayyid Muhammad bun Hamza iliyopo katika wilaya ya Hindiyya mkoani Karbala, siku ya Jumatatu saw ana tarehe (3/10/2022).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: