Kamati ya majaji wa shindano la zawadi ya vizito viwili katika uandishi wa msahafu mtukufu imechagua waandishi kumi wa kiiraq

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu imechagua waandishi kumi miongoni mwa wale walioshiriki kwenye shindano la zawadi ya vizito viwili, watapewa nafasi ya kushiriki kwenye uandishi wa msahafu wa kwanza, kwa mujibu wa matokeo ya mwisho ya majaji wa shindano hilo.

Shindano hilo limesimamiwa na kituo cha uchapaji wa Qur’ani tukufu chini ya Majmaa-Ilmi katika Atabatu Abbasiyya, majina ya watu kumi waliochaguliwa ni:

  • 1- Khalili Ahmadi Hussein Muntak / Arbiil.
  • 2- Haadi Kaadhim Naaif Daraji / Bagdad.
  • 3- Nabiil Hussein Farhani Ma’amuri / Najafu Ashrafu.
  • 4- Ali Muhammad Yunusi Abdulqadir / Nainawa.
  • 5- Karizan Abubakari Karim Afandi / Arbiil.
  • 6- Luqman Muhammad Yusufu / Karkuuk.
  • 7- Ibrahim Yaqub Alhiti / Ambaar.
  • 8- Alaa Abduljabaar Daudi Nasrawi / Bagdad.
  • 9- Samaan Kaka Diwana Hussein / Arbiil.
  • 10- Wasam Zaidani Saidi / Bagdad.

Muwakilishi wa kamati atawasiliana na waandishi hao kwa ajili ya kuwaambia wakati wa kuanza kuandika msahafu mtukufu chini ya taratibu na masharti yaliyowekwa na kamati ya usimamizi wa shindano.

Asilimia kubwa ya washiriki wa shindano hilo wametoka Bagdad, Dhiqaar, Baabil, Najafu, Karkuuk, Waasit, Ambaar, Arbiil, Karbala, Misaan, Suleimaniyya, Basra, Diwaniyya na Nainawa.

Tambua kuwa kuna washiriki walipata matokeo yanayo wawezesha kushiriki kwenye kazi ya uandishi wakati wowote iwapo mmoja katika wateule kumi atapata udhuru au akashindwa kushiriki kwenye zowezi la uandishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: