Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinashiriki kwenye kongamano la kwanza la maendeleo ya binaadamu

Ugeni kutoka kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya umeshiriki kwenye kongamano ya maendeleo ya kibinaadamu katika mji wa Baabil.

Kongamano hilo linahusu kuwajengea uwezo watumishi wa serikali katika mkoa wa Baabil, kwa kushirikiana na kituo cha mafunzo kutoka kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu idara ya afya ya Baabil, kauli mbiu ya kongamano hilo inasema (masomo mazuri kilele cha ubora).

Ugeni huo umewakilishwa na Sayyid Ali Hasuun Shimri, kiongozi mtendaji wa kitengo, Sayyid Karaar Hussein Ma’amuri kiongozi wa idara ya mafunzo.

Mada tofauti zimefundishwa kwenye kongamano hilo, ikiwa ni pamoja na mfumo wa ufundishaji katika serikali, uratibu wa kazi na ufanyaji wa tathmini.

Sambamba na mada za maadili na umuhimu wa kuwajengea uwezo madaktari wapya, athari za masomo kwa viongozi na wakuu wa idara na taasisi za afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: