Atabatu Abbasiyya imeanza kuomboleza kifo cha Imamu Askari (a.s)

Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Askari (a.s).

Kiongozi wa idara Shekhe Abduswahibu Twaiy amesema “Majlisi zinafanywa chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), unaohusika na kuadhimisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) likiwemo tukio hili chungu linalo ombolezwa siku hizi”.

Akasema kuwa “Majlisi itadumu kwa muda wa siku tatu, kuanzia siku ya Jumapili (2/10/2022) kila siku kunamihadhara miwili inayotolewa ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mhadhara wa asubuhi unatolewa na Sayyid Ali Hijazi na mhadhara wa jioni unatolewa na Shekhe Jafari Ibrahimi ikifuatiwa na muimbaji Muhammad Mu’tamadiy na Hassan Suruur”.

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza na imewekwa mapambo meusi kwa ajili ya tukio la kuomboleza msiba huo mkubwa, Alasiri ya Jumatano kutakua na matembezi ya maukibu ya Ataba mbili tukufu kwa ajili ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) sambamba na kupokea waombolezaji na mawakibu za kuomboleza.

Mihadhara inahusu mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na historia tukufu ya Imamu Hassan Askari na baadhi ya karama zake (a.s), namna alivyo pambana na changamoto za upotoshaji katika zama zake, kupitia mwenendo wake, nasaha na usia, aidha yanaelezwa mambo aliyofanyiwa na watawala wa bani Abbasi, kisha mhadhara unahitimishwa kwa kutaja tukio la kifo chake (a.s) kilichotokana na sumu kutoka kwa kiongozi muovu wa bani Abbasi aitwae Mu’tamad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: