Jopo la madaktari wa hospitali ya Alkafeel katika mji wa Karbala, limefanikiwa kuokoa mgonjwa asipooze kwa kumfanyia upasuaji wa kisasa kwenye uti wa mgongo.
Daktari bingwa wa ubaruaji wa uti wa ngongo, Dokta Iraani Muhammad Zaarai amesema “Tumefanikiwa kufanya upasuaji wa uti wa mgongo na kurekebisha pingili za uti wa mgongo pamoja na kupandikiza ute kwa mgonjwa aliyekua na tatizo hilo na alikua hawezi kutembea”.
Akaongeza kuwa “Mgonjwa alikua kwenye hatari ya kupooza, vipimo vimeonesha kuwa alikua na tatizo la pingili za uti wa mgongo” akasema: “Baada ya kumaliza matibabu mgonjwa ameondoka hospitali akiwa na afya njema”.
Tumefanikiwa kupandikiza ute kwa kutumia teknolojia ya kisasa na vifaa-tiba bora zaidi vilivyopo kwenye chumba cha upasuaji.