Kitengo cha usafiri kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu kinashiriki kubeba mazuwaru wa Imamu Hassan Askari (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake kwenye mji wa Samaraa kusini ya Bagdad.
Rais wa kitengo hicho Sayyid Abduljawadi Kaadhim amesema “Kitengo cha usafirishaji cha Atabatu Abbasiyya tukufu hushiriki kila mwaka kwenye shughuli za kuomboleza kifo cha Imamu Askari (a.s), kwa kutuma gari za kubeba mazuwaru, kuanzia basi za umma zinapo ishia hadi karibu na malalo takatifu”.
Akaongeza kuwa “Mara baada ya kuanza utekelezaji wa ratiba ya ziara na kuweka vituo vya ukaguzi kwa ajili ya kuimarisha usalama wa mazuwaru, pamoja na kubainisha sehemu za kuchukua mazuwaru zilizopangwa na kamati inayosimamia ziara, tulianza mara moja kutekeleza jukumu tulilopewa”.
Akafafanua kuwa “Tumetuma idadi kubwa ya gari zenye uwezo wa kubeba watu (24) na gari za kubeba wageni maalum”.