Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya nadwa ya kuwajengea uwezo watumishi wake wa tawi la wanawake

Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya nadwa ya kuwajengea uwezo watumishi wake wa tawi la wanawake yenye kauli mbiu isemayo “Mwanamke salama mtoto salama”.

Makamo rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Maitham Hamidi Qambari amesema “Maktaba kuu ya chuo imeandaa nadwa ya kuwajengea uwezo watumishi wa tawi la wanawake, chini ya uhadhiri wa Dokta Muhsin Mussa ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Washiriki wa nadwa hiyo ni watumishi wa kike wanaofanya kazi kwenye idara mbalimbali za chuo, mada zilizo tolewa zilikua zinahusu usalama wa mama na mtoto”.

Makamo rais wa chuo amesema kuwa “Zimetolewa nasaha mbalimbali za kiafya kwa wanawake na jinsi ya kulinda mtoto anapokua katika umri mdodo, sambamba na umuhimu wa lishe na namna inavyo saidia makuzi ya mtoto kihisia na kiakili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: