Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimepokea kundi la wanafunzi kutoka Bagdad chini ya program ya Multaqal-Qamaru.
Shekhe Mustwafa Idani mtafiti kutoka kitengo tajwa amesema “Kituo hufanya vikao vya kielimu wakati wote, leo tumekamilisha utoaji wa mihadhara kwa wageni kutoka mji wa Sha’alah jijini Bagdad”.
Akaongeza kuwa “Ratiba imepangwa kulingana na umri wa washiriki pamoja na kuzingatia kiwango cha elimu yao, mihadhara ilijikita katika kutatua changamoto za kinafsi na kijamii na kuwaandaa kielimu, kijamii na ki-imani”.
Kuhusu mada zilizo wasilishwa amesema kuwa “Kulikua na mada isemayo, kujenga mtu mwenye mafanikio, mada hiyo ilikua na vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kuangazia mambo yenye athari kwa mwanaadamu”.