Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kimetoa kitabu cha muongozo wa maonyesho ya turathi kimataifa toleo la pili

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapisha kitabu cha muongozo wa maonyesho ya kimataifa toleo la pili, kwa anuani isemayo (Tabia tukufu) maonyesho yanafanywa katika uwanja wa katikati ya haram mbili kwa ushiriki wa waandishi mahiri kutoka nchi tofauti.

Kitabu cha muongozo kimeandikwa mambo ambayo hufanywa kwenye maonyesho, kama vile warsha za kielimu, hafla ya ufunguzi na ufungaji, mabango yapatayo 86, yanayo onyesha mazingira ya maonyesho sambamba na kuonyesha hali halisi ya maonyesho mwanzo hadi mwinsho bila kuacha kitu chochote.

Kitabu hiki ni sehemu ya kutunza harakati zinazofanywa na kitengo, toka kilipo anzishwa kimekua kikikusanya shuhuda mbalimbali na kuzichapisha.

Kumbuka kuwa idara ya habari katika kitengo hiki, imekusanya shuhuda nyingi kupitia ofisi ya machapisho, na inashuhuda mpya zitatolewa hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, miongoni mwa shuhuda hizo ni: muongozo wa shindano la maarifa ya turathi awamu ya pili na muongozo wa turathi za Karbala na nyingineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: