Kitengo cha utumishi kimeandaa zaidi ya sanduku elfu (3) kwa ajili ya kutunza vitu vya mazuwaru

Kitengo cha utumishi kimeandaa zaidi ya sanduku elfu (3) kwa ajili ya kutunza vitu vya mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Makamo raisi wa kitengo hicho Sayyid Muhammad Harbi amesema “Idara ya sanduku ni moja ya ofiri za utunzaji wa amana katika kitengo cha utoaji wa huduma kwa mazuwaru hasa katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, hivyo kimeweka sanduku za kutunzia vitu pande zote za haram tukufu”.

Akaongeza kuwa “Idara imeweka utaratibu mzuri kwa mazuwaru kupata fungua za sanduku hizo kwa urahisi”, akafafanua kuwa “Tumeona tofauti kubwa baada ya kuruhusu wageni kuingia na simu ndani ya haram, msongamano wa watu kwenye mabanda ya kutunzia amana umepungua kwa kiwango kikubwa”.

Akafafanua kuwa “Kila mstari unasanduku (30) na kila sehemu zipo sanduku (105) hadi sasa jumla ya sanduku zote ni zaidi ya (3000)”.

Hakika kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara zake mbalimbali, kinahudumia mazuwaru wa mwezi wa bani Hashim (a.s) katika mji wa Karbala kwa muda wa saa (24) kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: