(Duraru Muhammadiyya).. Shindano linalofanywa sambamba na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume mtukufu

Idara ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa shindano la (Duraru Muhammadiyya) katika kuadhimisha kumbukumbu ya mazazi ya Mtume (s.a.w.w).

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na idara hiyo masharti ya shindano ni:

  • 1- Shindano ni kwa ajili ya wanawake pekee.
  • 2- Umri wa mshiriki usiwe chini ya miaka kumi na nne.
  • 3- Haifai kukopi moja kwa moja, majadiliano hayakatazwi.
  • 4- Matokea yatatangazwa siku ya mwezi (17 Rabiul-Awwal) sawa na tarehe (14/10/2022m) saa kumi jioni ndani ya sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s), kura itabigwa kupata majina ya washindi watano.

Tangazo linasema kuwa mshindi atakosa haki yake kama hatahudhuria kwenye hafla hiyo na kukosekana muwakilishi wake, mwisho wa kutuma majibu ni tarehe (12/10/2022m).

Shindano ni la kujibu maswali yanayohusu historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: