Makamo katibu mkuu amesema: Kazi ya kufunga dirisha jipya kwenye malalo ya Aqilah itakamilika ndani ya siku mbili zijazo

Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Abbasi Musawi Ahmadi, amesema kuwa ufungaji wa dirisha la kwenye malalo ya bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya umepiga hatua kubwa.

Makamo katibu mkuu alipoongea na vyombo vya Habari amesema kuwa “Kazi ya kufunga dirisha jipya kwenye malalo ya Aqilah imefika asilimia (80) na itakamilika ndani ya siku mbili zijazo”.

Akaongeza kuwa “Kazi ya kufunga dirisha hilo inasimamiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na inaenda kama ilivyo pangwa, wanafanya kazi usiku na mchana tangu dirisha hilo lilipofikishwa Sirya wiki mbili zilizopita”.

Kuhusu hafla ya ufunguzi wa dirisha hilo amesema kuwa, viongozi arubaini kutoka Atabatu Abbasiyya na watumishi zaidi ya mia saba watashiriki kwenye hafla ya ufunguzi, akasisitiza “Ushirikiano mzuri uliopo kati ya Ataba mbili tukufu Abbasiyya na Zainabiyya ambao ndio msingi wa kufanikisha kazi hii kwa urahisi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: