Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inafanya semina mpya kuhusu hukumu za usomaji

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina kuhusu hukumu za usomaji katika mkoa wa Najafu-Ashrafu.

Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi ya Qur’ani tukufu Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Semina inafanywa siku tatu kwa wiki kwa muda wa miezi miwili, jumla ya wanafunzi 20 wanashiriki kwenye semina hiyo”.

Akaongeza kuwa “Semina hii ni sehemu ya mkakati wa kielimu wa idara ya usomaji unaolenga kujenga tabia ya usomaji wa Qur’ani katika jamii”.

Maahadi inafanya semina mbili katika ofisi zake hivi sasa, wiki ijayo kuna semina zingine mbili zitaanza, moja ya hukumu za kusimama na kuanza, nyingine ya kujenga uwezo wa walimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: