Markazi Dirasaat Afriqiyya chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imepokea ugeni wa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kutoka Laiberia.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Hakika tunalipa umuhimu mkubwa swala la kuwasiliana na kushirikiana na watu wa bara za Afrika, sambamba na kuwapa kila aina ya msaada uliondani ya uwezo wetu katika kuendeleza Dini kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao”.
Akaongeza kuwa “Kituo hiki chini ya usimamizi na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kinafanya program nyingi, ikiwemo program ya kuchimba visima kwenye nchi kumi na tatu, mradi ambao umesaidia maelfu ya familia za Afrika kupata maji”.
Wageni wamesifu umuhimu wa Markazi (kituo) na wamepongeza kazi kubwa inayofanywa ya kueneza Dini katika bara la Afrika kwenye zaidi ya nchi kumi na tatu sambamba na kusaidia familia za waafrika waishio Iraq.
Akasisitiza kuwa “Tuna program mbalimbali katika bara la Afrika, ndani ya muda mfupi ujao tutakuwa na semina za Aqida, Qur’ani na Akhlaq kwenye nchi tofauti na miji tofauti ya Afrika”.