Kitengo kinachosimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kinaendelea na kazi ya kuvuna tende zilizopo katikati ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuzigawa kwa mazuwaru.
Makamo rais wa kitengo hicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Kaadhim Swalehe Mahadi amesema “Baada ya kuchuma tende na kuzikusanya sehemu moja husafishwa na kuwekwa kwenye vifungashio maalum kwa ajili ya kuzigawa kwa mazuwaru”.
Akaongeza kuwa “Uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu unaumuhimu mkubwa sana, miongoni mwa vitu vilivyopo kwenye uwanja huo ni mitende iliyopandwa kwa idadi ya miaka ya Imamu Hussein (a.s)”.
Mazuwaru wengi hujitokeza kuchukua tende zinazovunywa kwenye mitende hiyo, kwani mitende hiyo imepandwa eneo takatifu la katikati ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Mbeba bendera (a.s).