Wiki ya kwanza katika program ya kujenga uwezo wa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilika

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kimekamilisha wiki ya kwanza katika program maalum ya kujenga uwezo wa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ya kuhitimu imehudhuriwa na Mheshimiwa Sayyid Liith Mussawi mjumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu, na rais wa kamati inayosimamia program hiyo, wametoa maelekezo muhimu na nasaha kwa watumishi hao.

Sayyid Liith Mussawi ameeleza malengo ya program hiyo kuwa ni kujenga ushirikiano baina ya watumishi, sambamba na kuwajengea uwezo katika fani zao, halafu akasikiliza maoni ya watumishi na changamoto zao pamoja na kutoa njia za kutatua changamoto hizo.

Mwisho wa program hiyo washindi wakapewa zawadi, washiriki wamepongeza program na wakasema kuwa inafaida kubwa.

Tambua kuwa program za aina hii huandaliwa na kamati ya program za Atabatu Abbasiyya tukufu, hudumu kwa muda wa siku tano kwa kila kikundi, hufundishwa mambo mbalimbali, hutolewa mihadhara na mashindano pamoja na safari za utalii wa kidini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: