Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umetoa pole kwa familia ya mhudumu wa kujitolea kwenye kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu “Zainul-Aabidina Swabahu” aliyefariki wakati anahudumia mazuwaru wa arubaini ya Imamu Hussein.
Makamo rais wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili Sayyid Ahmadi Shaakir amesema “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tumekuja Basra kutoa pole kwa familia ya mhudumu wa kujitolea “Zainul-Aabidina Swabahu” aliyefariki wakati anahudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini”.
Shaakir akaongeza kuwa “Ugeni umetoa msaada wa kimaana na kimada kwa familia ya marehemu pamoja na kuwapa bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.