Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya hafla ya kuwapongeza washindi wa shindano la kuhifadhi Qur’ani tukufu mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Ataba tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.
Katika Halfa hiyo ujumbe kutoka uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliwasilishwa na Dokta Hassan Daakhil makamo kiongozi mkuu wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akabainisha umuhimu wa miradi ya Qur’ani inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Shindano lilifanyika kwa muda wa siku mbili na kupatikana washindi kutoka kwenye vikundi viwili katika hatua ya kwanza.
Maahadi hufanya semina za kuhifadhi na kusoma Qur’ani mara kwa mara, sambamba na kufanya hafla za kuwapongeza washindi na kuwapa zawadi kama sehemu ya kuwashajihisha kuendelea na masomo ya Qur’ani tukufu.