Kitengo cha zawadi na nadhiri kimemaliza kudarizi kitambaa cha makaburi mawili ya Maimamu wawili Askariyaini

Watumishi wa kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kazi ya kudarizi vitambaa vya kufunika kwenye makaburi mawili ya Maimamu – Askariyaini (a.s) na vitambaa vya kwenye makaburi mengine yaliyomo ndani ya malalo hiyo takatifu.

Kiongozi wa idara ya ushonaji Sayyid Abduzahra Daudi Suleiman amesema “Baada ya kupokea mchoro kutoka Atabatu Askariyya, tuliuingiza kwenye kompyuta na kuufanyia usanifu kisha tukaanza kudarizi”.

Akabainisha kuwa “Aina ya kitambaa tulichotumia ni (Qadifa nyeusi) ambacho tumepamba juu yake kwa kudarizi aya za Qur’ani tukufu”, akaongeza kuwa “Kitambaa kimoja kinaupana wa (180 sm) na urefu wa (95 sm), tutafunika kaburi nne ambazo ni (kaburi ya Imamu Askari na Imamu Haadi (a.s), sambamba na kaburi la bibi Hakima na bibi Fidha, kila kaburi litafunikwa na vitambaa vine”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Abduzahra, muda wa kazi hiyo utakuwa mwezi kamili, vitambaa vilivyopo kwenye kaburi hizo vitatolewa mwezi wa Muharam mwaka kesho na kuwekwa vitambaa vipya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: