Uongozi wa Wakfu-Shia umesema: Utengenezaji wa dirisha jipya la malalo ya Aqilah ni kuonyesha utiifu na mapenzi ya dhati kwa bwana wa mashahidi

Rais wa uongozi wa Wakfu-Shia Dokta Haidari Shimri amesema kuwa utengenezaji wa dirisha jipya la malalo ya Aqilah ni kuonyesha utiifu na mapenzi ya dhati kwa Imamu Hussein (a.s).

Ameyasema hayo jioni ya siku ya Jumamosi kwenye hafla ya ufunguzi wa dirisha jipya la malalo ya kiongozi wa Sham bibi Zainabu (a.s) iliyofanywa ndani ya haram tukufu ya Zainabiyya.

Akaongeza kuwa “Hauwezi kupima kiwango cha mapenzi na utiifu kwa kuangalia kaburi au jengo, hakika Ahlulbait (a.s) ndio mlango wa Mwenyezi Mungu anaotumia kutoa, hongera sana kwa waliojitolea na kushiriki kwenye mradi huu mtukufu”.

Katika ujumbe huo Mheshimiwa Shimri ametoa shukrani maalum kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini na watumishi wote wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walioshiriki kwa nyoyo zao, ndimi zao na mikono yao mitukufu, akasifu ubora na uzuri wa dirisha hilo tukufu ambalo sasa limewekwa kwenye kaburu takatifu la Hauraa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: