Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani asubuhi ya Jumapili amepokea ugeni kutoka taasisi ya kijamii Al-Ain uliongozwa na rais wa taasisi hiyo Sayyid Ahmadi Sudani na baadhi ya watumishi wake.
Ziara hiyo ni kwa ajili ya kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Marjaa mkuu kutokana na kuonyesha kwake Imani kwa taasisi hiyo na kusaidia shughuli zake za kitaifa na kimataifa.
Mheshimiwa Sayyid Sistani amepongeza utendaji wa taasisi hiyo na kuitakia mafanikio mema katika kuhudumia mayatima, akasema kuwa taasisi inaonyesha picha nzuri kwa wahisani, aidha akasisitiza umuhimu wa kuwaonganisha wanufaika kwenye jamii, Dini na maadili mema.
Taasisi ya kijamii Al-Ain ni miongoni mwa taasisi za kijamii, ilianzishwa mwaka 2006, imepewa baraka na kuridhiwa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, inahudumia mayatima na mafakiri katika nyanja tofauti za Maisha yao.