Kitengo cha utumishi kimesema: Jukumu la kudumisha usafi katika Atabatu Abbasiyya na maeneo yanayo zunguka Ataba ni endelevu

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya usafi siku zote katika haram tukufu na kwenye barabara zinazozunguka eneo hilo takatifu.

Makamo rais wa kitengo hicho Mhandisi Abbasi Ali, amesema: “Miongoni mwa majukumu ya kitengo cha utumishi ni kusafisha jengo la haram tukufu na barabara zinazo zunguka jengo hilo, kama barabara ya Alqami, Hauraa, Qamaru, Shuhadaa, Imamu Ali na barabara ya Kibla ya Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Gari za taka hubeba tani 10 hadi 15 za taka kila siku kutoka eneo hilo na Kwenda kuzitupa nje ya mji”.

Akaendelea kusema “Watumishi husafisha na kutandika mazulia ndani ya haram na kwenye vibaraza vinavyo zunguka haram takatifu kwa kushirikiana na idara ya mitambo iliyochini ya kitengo hicho”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: