Nchini Kamerun.. kitengo cha Habari na utamaduni kinaadhimisha mazazi ya wakweli wawili (a.s)

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinasherehekea mazazi ya Mtume Muhammad na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s) kupitia hafla iliyofanywa nchini Kamerun na kuhudhuriwa na kiongozi wa umma Mheshimiwa Sayyid Hassan Sanko.

Hafla ya maadhimisho hayo imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Hafla ilikua na vipengele vingi ikiwa ni pamoja na kueleza mwenendo wa uislamu na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na historia ya Maisha yake na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Hafla imetaja mazazi ya Mtume mtukufu (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Swadiq (a.s) nchini Kamerun, imehudhuriwa na wafuasi wengi wa Ahlulbait (a.s) bila kumsahau kiongozi wao Mheshimiwa Sayyid Hassan Sanko, na kundi la mubalighina na viongozi wa makabila katika taifa la Kamerun”.

Akaendelea kusema “Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya imegawa chakula kwa watu wote walio hudhuria baada ya hafla hiyo tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: