Rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu: Tunaendelea kulinda mafanikio yaliyopatikana

Rais wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu Dokta Mushtaqu Ali amesema kuwa Hakika Majmaa inalinda mafanikio yaliyopatikana kupitia maahadi za Qur’ani kwa kufanya miradi ya Qur’ani.

Ameyasema hayo alipokutana na watumishi wa Maahadi ya Baabil na Hindiyya zilizo chini ya Majmaa katika kulinda viwango vya walimu.

Katika kikao hicho amesisitiza ulazima wa kufuata maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na usia wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, akasema kuwa lengo kuu ni kurudisha jina la “Imetengenezwa Iraq” kwenye kila kitu.

Akaongeza kuwa “Hatua ijayo ni bora zaidi na ya kujivunia katika miradi ya Qur’ani itakayofanywa na Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: