Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha semina ya Qur’ani katika kanuni za tajwidi.
Semina hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi.
Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi Sayyid Ahmadi Zaamili amesema “Semina imefanywa katika chuo cha Ankushi kwenye mtaa wa Alwafaa, kwa ushiriki wa wanafunzi ishirini, wamefundishwa masomo ya nadhariyya na vitendo yanayo husu kanuni za tajwidi kwa muda wa miezi mitatu chini ua Ustadh Tofiq Salami”.
Akaongeza kuwa “Maahadi inafanya semina tatu kwa sasa, zinazo husu kanuni za tajwidi, kusimama, kuanza na usomeshaji sahihi katika ofisi za Najafu tukufu”.
Akabainisha kuwa “Harakati zote zinazo husu Qur’ani zipo katika mkakati wa kuboresha usomaji wa Qur’ani na kuongeza idadi ya wasomaji, mahafidh na wafasiri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu kitakatifu”.