Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel, limefanikiwa kuokoa Maisha ya mtoto mwenye umri wa siku mbili aliyekua na tatizo kwenye utumbo mnene.
Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto, Dokta Samad Rabii amesema “Mtoto alikua na tatizo kubwa kwenye utumbo mnene, tatizo ambalo ni adimu kutokea na husababishwa na mambo mengi”.
Akasema: “Mtoto aliingizwa haraka kwenye chumba cha upasuaji, kwa ajili ya kuokoa Maisha yake kwa kumfanyia upasuaji wa tumbo na kuondoa tatizo, sambamba na kupangilia utumbo na kuhakikisha anaendelea na Maisha kama kawaida”