Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inaendeleza vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya Maqaam ya Imamu wa zama (a.f)

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, inaendelea kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu ndani ya Maqaam ya Imamu wa zama (a.s) kila siku jioni baada ya swala ya Isha.

Vikao hivyo vinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Karbala, kwa mujibu wa maelezo ya Shekhe Ali Rawii.

Akaongeza kuwa “Kwenye vikao hivyo hufafanuliwa kukumu za usomaji na kubainisha makosa yanayofanywa na wasomaji wengi wa Qur’ani na njia sahihi ya usomaji”.

Akasema: “Tunahitimisha Qur’ani nzima kwa muda wa miezi minne, ratiba hii tunaifanya pia kwenye mikoa mingine”.

Akaongeza kuwa “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinapata muitikio mkubwa kutoka kwa waumini na wakazi wa maeneo yanayozunguka Maqaam tukufu pamoja na mazuwaru”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: