Atabatu Abbasiyya imeonyesha mradi wa kuendeleza mji mkongwe wa Karbala

Siku ya Jumamosi Atabatu Abbasiyya tukufu imeonyesha mradi wa kuboresha mji mkongwe wa Karbala, wahandisi wamesema wataanza kutekeleza hatua ya kwanza ya ujenzi wa uwanja wa haram ya Ummul-Banina (a.s).

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi, Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amekiambia kituo cha habari kuwa "Mradi wa ujenzi wa mji mkongwe wa Karbala ulisanifiwa tangu mwaka (2014m)", akaongeza kuwa “Mradi huo umepasishwa na wizara ya mipango miji, mkoa wa Karbala, ofisi ya mipango ya ujenzi, kisha Atabatu Abbasiyya ikaanza utekelezaji wa hatua ya kwanza kwa kununua ardhi na nyumba zilizopo katika eneo la mradi”.

Akasema “Wahandisi wetu wameanza hatua ya kwanza ya ujenzi wa uwanja wa haram ya Ummul-Banina (a.s) upande wa kaskazini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akafafanua kuwa “Hatua ya kwanza ya mradi inahusisha kuvunja nyumba zilizopo eneo hilo na kuondoa miungombinu ya maji na umeme, na kuhakikisha sehemu inakuwa wazi kwa ajili ya ujenzi wa msingi”, akasema: “Eneo la mradi linaukubwa wa mita elfu 20, inatarajiwa kujengwa sardabu (handaki) kubwa katika eneo hilo, huku eneo la juu likijengwa na kupauliwa kwa ajili ya kivuli kwa mazuwaru watukufu”.

Rais wa kitengo akasema “Mradi huo utakua namlango mkubwa upande wa uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”, akasema “Hatua zingine zinaendelea hadi mwisho wa mradi, ikiwa ni pamoja na kuendelea kununua nyumba zilizopo kwenye eneo la mradi”.

Mradi umesanifiwa na wataalam wa kitengo cha miradi ya kihandisi, akasisitiza kuwa “Mradi umeanza kutekelezwa baada ya kupasishwa na wakfu Shia na wizara ya mipango chini ya shirika la ujenzi la kiiraq la Ardhi takatifu, na wahisani ni ofisi ya Wakfu-Shia na wizara ya mali na mipango”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: