Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na mradi wa Qur’ani (Watafakari aya zake), kwenye misikiti kadhaa ya mji wa Karbala.
Mradi huo unatekelezwa ndani ya misikiti na husseiniyya zilizopo kwenye vitongoji na mitaa tofauti hapa mkoani.
Mradi unalenga kutoa elimu ya Qur’ani katika jamii na kuelezea vizito viwili vitakatifu sambamba na kuhuisha misitiki kwa kufanya vikao vya usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu.