Kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kirkuk.. Atabatu Abbasiyya imefanya kongamano la mazazi ya Mtume mtukufu

Uomgozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kirkuk umefanya kongamano la kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ndani ya eneo la chuo.

Kongamano limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Muhammad Ibrahim, ikafuatiwa na wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu.

Ujumbe wa rais wa chuo cha Kirkuk Dokta Imran Jamali umewasilishwa kwenye kongamano hilo, amesema: “Hakika leo tunaadhimisha mazazi ya mbora wa walimwengu, ambaye hakuja kwa mji maalum au taima maalum, bali kwa ulimwengu mzima na watu wote yeye ni rehema ya walimwengu, akaeleza umuhimu wa kufuata mafundisho yake matukufu”.

Akaongeza kuwa “Kutokana na tukio hili tukufu tunapongeza chuo kikuu cha Kirkuk na watumishi wake wote kwa kuingia katika mfumo wa kiarabu na kimataifa”.

Ukafuata ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu uliowasilishwa na Dokta Ahmadi Shekhe, akasema: “Uislamu umetukuka kwa nuru ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) tangu alipozaliwa hadi leo, nuru imeongezeka na ujinga umepungua duniani, yatupasa tuadhimishe mazazi ya Mtume mtukufu wakati wote na kila mahala, hakika yeye ni shule kwa walimwengu wote”.

Akaendelea kusema “Leo ni siku ya kuhadithia kisa cha kuzaliwa kwake, miujiza yake, jinsi alivyo anza kulingania uislamu na kujadili mafanikio yanayoweza kupatikana kwa watu kufuata mwenendo wake na mafundisho yake matakatifu”.

Kongamano limepambwa na tenzi zilizosomwa na Haidari Mussawi na Muhammad Tamimi.

Kongamano likahitimishwa kwa kugawa zawadi kwa wanafunzi wanaovaa Abaa ya Kiiraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: