Katika mkoa wa Diwaniyya.. Ugeni kutoka Majmaa-Ilmi umehudhuria hafla ya ufunguzi wa Maahadi ya Qur’ani

Ugeni kutoka Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya umehudhuria kwenye kongamano la ufunguzi wa Maahadi ya Imamu Swadiq (a.s) ya masomo ya Qur’ani katika mkoa wa Diwaniyya chini ya kamati ya Imamu Swadiq (a.s) ya utamaduni.

Hafla hiyo imesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa-Ilmi.

Kiongozi wa kamati Shekhe Basim Waailiy amesema “Maahadi Imamu Swadiq (a.s) ya masomo ya Qur’ani na shule ya kidini, zinaunda kamati ya Imamu Swadiq (a.s) inayolenga kutoa elimu ya vizito viwili Kitabu na kizazi kitakatifu”.

Akaongeza kuwa “Kamati hufanya harakati mbalimbali, yakiwemo makongamano ya kuadhimisha matukio tofauti ya kidini, kama kumbukumbu za kuzaliwa kwa Maimamu watakatifu (a.s) na kumbukumbu za vifo vyao (a.s), katika maadhimisho hayo hutolewa mafunzo ya kidini, kijamii, kitamaduni na mengineyo”.

Hafla ya ufunguzi imehudhuriwa na viongozi wa hauza kutoka Najafu, ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya, ugeni kutoka taasisi za Qur’ani pamoja na waumini wanaoishi maeneo ya jirani na hapa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: