Kitengo cha maarifa: Tunafanya kila tuwezalo katika kutunza turathi za Karbala

Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia kituo cha turathi za Karbala kinacho jihusisha na turathi za Karbala kimesema, tunafanya kila tuwezalo kutunza turathi za Karbala.

Mkuu wa kituo Dokta Ihsani Gharifi amesema “Toka kuanzishwa kwa kituo hadi sasa, tunafanya kila tuwezalo kutunza turathi za Karbala na kuzitangaza”.

Akaongeza kuwa “Kituo kimefungua madirisha tofauti kwa ajili ya kuhakiki na kuthibitisha turathi za Karbala, sambamba na kuanzisha jarida kwa jina la (Turathi za Karbala), kwenye jarida hilo kuna Makala zinazo andikwa na watafiti mbalimbali wa kisekula, aidha kuna jarida lingine linaitwa (Turathi za Karbala zilizoandikwa), ambalo linajikita katika kukusanya barua na maandishi yaliyoandikwa na wanachuoni wa zamani, tumesha kusanya nakala-kale nyingi hadi sasa kituo kimekua kimbilio la watafiti na waandishi”.

Kuhusu mkakati wa baadae amesema: “Mwanzoni mwa mwaka kesho kituo kitafanya kongamano la pili kwa jina la (turathi zetu utambulisho wetu), tutaangazia turathi zetu na wanachuoni wa karne ya kumi, tafiti mbalimbali za kitaifa na kimataifa zitawasilishwa kwenye kongamano hilo, miongoni mwa nchi zitakazo shiriki ni Misri, Sirya, Iran na nchi zingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: